• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji wakimbia soko la madeni la Kenya huku kiwango cha riba kikipungua

    (GMT+08:00) 2014-09-02 11:20:15

    Wawekezaji mbalimbali wamekimbia soko la madeni la Kenya huku dhamana za serikali za muda mfupi zikiporomoka hadi kiwango cha chini kabisa. Kiwango cha riba kimepungua kwa wastani wa asilimia 8.

    Katika mnada uliofanyika Agosti 28, mapato ya dhamana za serikali za siku 91 yalishuka kwa alama 0.009 na kufunga wiki ikiwa na asilimia 8.2. Kiwango hicho cha chini kimefanya wawekezaji kukimbia soko la madeni katika wiki chache zilizopita. Wachambuzi wanasema wataendelea kuwa makini katika kuingiza pesa kwenye soko la madeni kwa vile kiwango cha riba kinaendelea kushuka.

    Benki za biashara, ambazo katikati ya mwezi Agosti zilikuwa na asilimia 53.5 ya jumla ya madeni ya serikali, wameyapunguza na kuwa takriban asilimia 53. Deni la jumla la Kenya kwa sasa ni dola bilioni 14.6, ambalo limeongezeka kutoka dola bilioni 14.1 la mwezi Juni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako