• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa nchi sita za Afrika kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika kuhusu ugaidi

    (GMT+08:00) 2014-09-02 11:35:28

    Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema marais wa Chad, Niger, Nigeria, Somalia, Tanzania na Uganda wamethibitisha kuwa watahudhuria mkutano wa kilele wa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika utakaofanyika mjini Nairobi, Kenya.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema lengo la mkutano huo ni kupitia hali na maendeleo ya juhudi za Umoja wa Afrika katika mapambano dhidi ya ugaidi

    Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema mkutano huo unatarajiwa kufikia makubaliano kuhusu hatua halisi za kuhimiza utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika katika mapambano dhidi ya ugaidi katika ngazi ya taifa, kanda na bara.

    Katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Juni mjini Malabo, Guinea ya Ikweta, viongozi wa nchi za Afrika walionesha wasiwasi wao kuhusu kuendelea kwa tishio la ugaidi barani Afrika, hasa katika maeneo ya Sahel Sahara, pembe ya Afrika na Afrika ya kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako