• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa wito wa kuongeza nguvu ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2014-09-11 18:01:33

    Rais Xi Jinping wa China amewasili Dushambe, mji mkuu wa Tajikistan, ambako atahudhuria mkutano wa 14 wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO, na baadaye atafanya ziara nchini Tajikistan, Maldives, Sri Lanka, na India. Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhimiza diplomasia ya ujirani ya China inayohusiana na kujenga ujirani wenye maridhiano, utulivu, na mafanikio, na kusimamia kanuni za uhusiano mwema, uaminifu, kunufaishana na kushirikiana.

    Rais Xi kuhudhuria mkutano wa SCO ni tukio muhimu katika ziara yake. Jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2001, imeendelea kukua na kuwa nguvu muhimu katika kulinda amani ya kikanda, na kuhimiza maendeleo ya pamoja. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa SCO walitoa waraka wa mkakati utakaoongoza maendeleo ya jumuiya hiyo hadi mwaka 2025. Katika mkutano unaofanyika leo, viongozi wa nchi hizo wataweka mkazo zaidi kwenye mkakati huo kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu ya SCO. Katibu mkuu wa kituo cha utafiti cha SCO kilicho chini ya chuo kikuu cha sayansi ya jamii cha China Sun Zhuangzhi amesema, mkakati huo wa maendeleo utafanya kuwe na ufuatiliaji wa kina kwenye maeneo mbalimbali ya ushirikiano.

    Denis Tyurin, mkurugenzi wa klabu ya biashara ya SCO amesema, mkakati huo utapanga maendeleo ya baadaye ya Jumuiya hiyo, na kuamua mwelekeo wa baadaye wa vipaumbele vya SCO. Naye naibu mkurugenzi wa chuo kikuu cha India cha elimu kuhusu China Jabin Thomas Jacob amesema, mkutano huo pia utapitisha nyaraka za kisheria za kupanua zaidi jumuiya hiyo, ambayo ni alama ya kuongezeka kwa ushawishi na kuvutia zaidi.

    Usalama na uchumi ni usukani unaoendelea kuisukuma mbele jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai. Tangu kuanzishwa kwake, nchi wanachama zimeendelea kuongeza nguvu ya kuaminiana kisiasa na ushirikiano wa kiuchumi. Thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi nyingine wanachama wa SCO imeongezeka kutoka dola bilioni 10 za kimarekani hadi kufikia dola bilioni 100 za kimarekani.

    Wakati wa mkutano wa mwaka 2013 wa Bishkek, rais Xi Jinping wa China alipendekeza makubaliano ya kuwezesha ujenzi wa barabara ya kimataifa ndani ya nchi wanachama wa SCO. Barabara hiyo ina lengo la kujenga njia zitakazounganisha bahari ya Baltic na ile ya Pasific, na kuunganisha Asia ya kati na bahari ya Hindi pamoja na Ghuba. Viongozi wa nchi wanachama wa SCO wanatarajiwa kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano haya wakati wa mkutano huu.

    Katibu mkuu wa shirikisho la elektroniki la China na Russia Sergey Sanakoev amesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo kutakuwa ni sehemu muhimu ya mapendekezo ya rais Xi ya kujenga ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri, na nchi wanachama wa SCO zitanufaika na makubaliano hayo.

    Kutokana na mawasiliano na maingiliano, China na nchi jirani zimeunda jumuiya yenye mustakbali wa pamoja. Ziara ya rais Xi kwenye nchi nne za Asia ni hatua nyingine muhimu ya kidiplomasia ya kuendeleza uhusiano kati ya China na nchi jirani na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako