• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Anhui machoni mwangu

    Nilipata fursa ya kuwa mmoja kati ya waandishi wa habari kutoka CRI walioshiriki kwenye ziara mkoani Anhui. Katika ziara hiyo, tuliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya kiuchumi pamoja na vivutio vya utalii katika miji ya Hefei, Wuhu, Anqing, pamoja na Huangshan.

    Mji wa Hefei ni mji unaokua kwa kasi kiuchumi, na pia kwenye sekta ya utalii mji huo una vivutio kadhaa. Kilichonivutia zaidi mjini humo ni eneo la ardhi lililopandwa miti na kutengenezwa kuwa kivutio cha utalii linaloitwa Bustani ya msitu oevu ya Binhu (Binhu wetland forest park) iliyo karibu na Mto Chaohu. Nilistaajabu kwa kuwa miti hiyo imepandwa kwa utaratibu, na pia maeneo yametengwa kwa wale wanaopenda kutembelea bustani hiyo kwa kutumia baskeli na vigari. Ujenzi wa msitu huo bado unaendelea, na utakapokamilika, bustani hiyo itakuwa ni sehemu nzuri sana ya kutembelea.

    Mji wa Hefei
    • Hefei
    Awali, mji wa Hefei ulijulikana kama Ho-fei, Luzhou, au Luchow, na mji mkuu wa mkoa wa Anhui ulioko mashariki mwa China. Mji huo wenye ngazi sawa na wilaya, ni makao makuu ya kisiasa, kichumi, na kiutamaduni ya mkoa wa Anhui. Mji wa Hefei unapakana na Huainan upande wa kaskazini, upande wa kaskazini mashariki unapakana na Chuzhou, kusini mashariki unapakana na Chaohu, na magharibi, mji huo unapakana na Lu'an....
    More>>

    • Mwandishi wetu wa habari Caroline Nassoro atembelea Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya China

    • Ziwa Tian'e mjini Hefei
    More>>
    Mji wa Wuhu
    • Wuhu
    Wuhu ni mji ulioko kusini mashariki mwa mkoa wa Anhui, na mji huo una hadhi sawa na wilaya. Ukiwa kusini mashariki mwa Mto Yangtze, Wuhu umepakana na Xuancheng upande wa kusini mashariki, Chizhou na Tongling upande wa kusini magharibi, Hefei kaskazini magharibi, Ma'anshan upande wa kaskazini mashariki, na mkoa wa Jiangsu upande wa mashariki. Idadi ya watu mjini Wuhu ni milioni 3,443,192 kutokana na sensa ya mwaka 2010....
    More>>

    • mwandishi wetu wa habari Caroline Nassoro atembelea mji wa Wuhu

    • Kijiji cha Xiangshuijian mjini Wuhu
    More>>
    Mji wa Anqing
    • Anqing
    Anqing ni mji wenye ngazi sawa na wilaya ulioko kusini magharibi mwa mkoa wa Anhui. Unapakana na Lu'an upande wa kaskazini, Hefei na Wuhu upande wa kaskazini mashariki, Tongling upande wa mashariki, Chizhou upande wa kusini mashariki, mkoa wa Jiangxi upande wa kusini, na upande wa magharibi, mkoa wa Hubei. Mji wa Anqing ni muhimu kwa viwanda vya nguo, spea za magari, chakula, na chai....
    More>>

    • Carol atembelea jumba la makumbusho ya opera ya Huangmei mjini Anqing, mkoani Anhui

    • Mlima Tianzhu mjini Anqing
    More>>
    Mji wa Huangshan
    • Huangshan
    Huangshan ni mji ulio kwenye milima iliyoko kusini mwa mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. Mji huo umejengwa kwenye milima inayotokana na vitu vilivyotolewa baharini wakati wa enzi za Mesozoi, miaka milioni 100 iliyopita. Mji huo ni maarufu kutokana na mandhari yake nzuri....
    More>>

    • Mwandishi wetu wa habari Caroline Nassoro

    • Milango ya kumbukumbu katika kijiji cha Tangyue
    More>>
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako