• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya siku ya kwanza ya hisa za Kampuni ya Alibaba ya China yavunja rekodi

    (GMT+08:00) 2014-09-19 18:52:30

    Kampuni ya biashara kupitia mtandao wa Internet Alibaba imeanza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa la Marekani kwa mafanikio, mafanikio ambayo wachambuzi wanaona yatatoa fursa mpya kwa wawekezaji dunia kunufaika na ukuaji wa uchumi wa China. Mauzo ya siku ya kwanza ya hisa za kampuni hiyo ilikuwa dola za kimarekani 68 na katika siku ya kwanza kampuni hiyo ilikusanya dola za kimarekani bilioni 21.8 na kuvunja rekodi katika mauzo ya siku ya kwanza katika historia ya Marekani.

    Mafanikio ya mauzo ya siku ya kwanza ya hisa za kampuni ya Alibaba yamewashangaza wengi. Wachambuzi wengi wa mambo ya soko la hisa wanakubaliana kuwa bei ya hisa hizo ilipaswa kuwa kubwa. Mchambuzi wa kampuni ya JG capital Bw Henry Guo anaona bei ya siku ya kwanza kwenye soko ya hisa ya kampuni ya Alibaba ni ndogo, kwa maoni yake ilipaswa kuwa dola za kimarekani 95.

    Lakini cha muhimu zaidi ni kuwa kuvutia kwa hisa za kampuni ya Alibaba kunatokana na imani ya wawekezaji wa kimataifa kuhusu uchumi wa China. Bw Guo amesema kwa sasa Kampuni ya Alibaba ni chaguo la kwanza kwa wawekezaji wa kimataifa wanaotaka kunufaika na maendeleo ya China. Kwa sababu Kampuni hiyo ina misingi imara, inakua kwa kasi na faida yake imewavutia wawekezaji.

    Mwaka jana kampuni ya Alibaba ilishughulikia biashara yenye thamani ya dola bilioni 250 za kimarekani, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko biashara zilizofanywa na kampuni kama hiyo, za Amazon na eBay kwa pamoja.

    Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya O'Neil kwenye soka la hisa la New York Bw Kenneth Polcari, amesema kwa wanaoamini kinachotokea duniani kwa sasa, na kama wanaamini kuwa uchumi wa China unaelekeza zaidi kuwa uchumi wa soko, fursa za kampuni ya Alibaba kwa siku za baadaye ni nzuri sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako