• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza uwekezaji wa dola bilioni 20 za kimerekani nchini India katika miaka mitano ijayo

    (GMT+08:00) 2014-09-19 20:05:25

    China imetangaza kuwa itaongeza uwekezaji wake nchini India katika sekta ya viwanda na ujenzi wa miundo mbinu hadi kufikia dola bilioni 20 za kimarekani katika miaka mitano ijayo.

    Lengo hilo limetangazwa katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi hizo mbili katika siku ya mwisho ya ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini India.

    Taarifa hiyo imesisitiza ahadi za nchi hizo mbili kubwa barani Asia za kuimarisha zaidi uhusiano kati yao.

    China pia imetangaza kuanzisha maeneo mawili ya kiviwanda katika sehemu ya magharibi mwa India.

    Siku hiyo rais Xi amekutana na viongozi mbalimbali wa India, wakiwemo spika wa bunge Sumitra Mahajan, mwenyekiti wa chama cha the Indian National Congress Sonia Gandhi, pamoja na aliye kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Manmohan Singh.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako