Waziri mkuu wa Uingereza Bw David Cameron amesema Scotland itapewa madaraka zaidi katika kujiamulia mambo yake, na sehemu nyingine za Uingereza pia zitapewa madaraka zaidi.
Kauli ya Bw. Cameron imekuja baada ya wanaopinga Scotland kujitenga na Uingereza kushinda kura za maoni kwa kupata asilimia 55.42, huku waliokuwa wanaunga mkono kujitenga wamepata asilimia 44.58 ya kura zilizopigwa.
Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso akizungumzia matokeo ya kura hizo za maoni amesema Scotland kubaki Uingereza kuna manufaa kwa umoja na nguvu ya Umoja wa Ulaya.
Akizungumzia matokeo ya kura hizo za maoni, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hong Lei amesema China inaona kuwa kura hizo za maoni ni mambo ya ndani ya Uingereza, kwa hiyo haitoi maoni juu yake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |