• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama laitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono Iraq katika vita dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2014-09-20 19:20:26

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana lilmeitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono serikali ya Iraq katika mapambano dhidi ya kundi la ISIS na makundi mengi ya kigaidi.

    Kwenye taarifa yake, baraza hilo limepongeza kuundwa kwa serikali mpya ya Iraq, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono zaidi katika kuimarisha mfumo wa kidemokrasia, kuhakikisha usalama unarudishwa nchini humo. Pia baraza hilo limeitarajia serikali hiyo mpya iweze kutatua matatizo ya nchi hiyo kwa kupitia mchakato wa kisiasa unaoshirikisha pande zote.

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi ameeleza kuwa, China inaiunga mkono Iraq kithabiti katika kulinda mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi yake, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha umoja na ushirikiano, ili kusukuma mbele maendeleo nchini Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako