• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China amaliza ziara katika nchi 4 za Asia ya kati na kusini

    (GMT+08:00) 2014-09-20 19:30:48

    Rais Xi Jinping wa China amerudi Beijing baada ya kuhudhuria mkutano wa 14 wa wakuu wa Jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai SCO na kumaliza rasmi ziara yake katika nchi nne za Tajikistan, Maldives, Sri Lanka na India.

    Akizungumzia ziara hiyo, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, nchi hizo nne ambazo zote ziko kwenye njia ya hariri ya kale na zimekuwa na husiano mzuri na China tangu zamani, ni vituo muhimu vya ruwaza ya kujenga ukanda wa kiuchumi wa njia za hariri ikiwemo ya baharini. Ziara ya rais Xi imeunganisha matumaini ya watu wa nchi hizo kwa ruwaza hiyo, na kushirikisha nchi hizo katika kuhimiza maendeleo na kutimiza amani na ustawi wa pamoja.

    Bw. Wang Yi amesema, ujirani mwema ni msingi muhimu wa ustawi wa China, na kuwa maendeleo ya China hayawezi kuondokana na mazingira yenye utulivu na amani, na pia yatatoa fursa za ushirikiano kwa nchi jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako