• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yasaini mkataba wa ukarabati wa barabara na kampuni ya China

    (GMT+08:00) 2014-09-21 19:08:19

    Mamlaka ya Ujenzi wa barabara ya Ethiopia ERA imesaini mkataba na kampuni ya ujenzi ya China utakaoiwezesha kampuni hiyo kutekeleza mradi wa ukarabati wa barabara ya kutoka Konso kwenda Yabello nchini Ethiopia.

    Mkataba huo ulisainiwa kati ya mkurugenzi wa ERA Zaid Wolde-Gebriel na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya China Tiesiju Civil Engineering Group LTD Bw Cai Xiaobin katika makao makuu ya ERA mjini Addis Ababa Ethiopia.

    Barabara hiyo ya kilomita 107 itakarabatiwa upya kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 6 na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 42. Bw Gebriel amesema ana imani kuwa kampuni hiyo ya China itakamilisha mradi huo ndani ya muda uliowekwa. Kwa upande wake, Cai amesema kampuni yake imejitolea kukamilisha mradi huo kwa wakati uliowekwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako