• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Obama ashutumiwa kutokana na ujumbe wake wenye utata wa kukabiliana na kundi la ISIS

    (GMT+08:00) 2014-09-21 19:08:56

    Wakosoaji wa Marekani wameendelea kumshambulia rais Barack Obama wa Marekani kufuatia ujumbe wake wa kujichanganya kuhusu vitisho vya kundi la ISIS na jinsi Marekani inavyojiandaa kupambana na kundi hilo.

    Serikali ya Obama ina wasiwasi kuwa kundi la ISIS litaweka ngome yao mashariki ya kati kabla ya kuishambulia Marekani kama tu kundi la Al-Qaeda lilivyofanya wakati wa shambulizi la Septemba 11 mwaka wa 2001 katika miji ya New York na Washington nchini Marekani.

    Katika miezi ya hivi karibuni, Kundi la ISIS limekuwa likipanua ngome yao kaskazini mwa Iraq na kuendeleza mapigano nchini Syria wakiwa na lengo la kuanzisha taifa lao la kiislamu. Serikali ya Obama imekuwa ikijipata pabaya kutokana na ujumbe usioeleweka jinsi ya kukabiliana na kundi hilo la ISIS. Hata hivyo Obama amesisitiza kuwa sera yake kuhusu ISIS bado hazijabadilika na kuongeza kuwa hana nia ya kutuma kikosi cha ardhini kupambana na kundi hilo la ISIS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako