• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wagombea urais wa Afghanistan wasaini makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

    (GMT+08:00) 2014-09-21 19:23:25

    Wagombea wawili wa urais wa Afghanistan wamesaini makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo, ambayo yanatoa nafasi kwa rais mpya kutangazwa.

    Wagombea hao ambao ni waziri wa fedha wa zamani Bw. Ashraf Ghani Ahmadzai na waziri wa mambo ya nje wa zamani Bw. Abdullah Abdullah walisaini makubaliano hayo jana, baada ya miezi kadhaa ya mgogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi April na Juni mwaka huu.

    Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Bw. Ashraf Ghani ndio rais mpya, huku mpinzani wake Abdullah Abdullah akimchagua afisa mkuu wa serikali atakayekuwa na madaraka kama yale ya waziri mkuu. Rais wa sasa Bw. Hamid Karzai amepongeza makubaliano hayo, na kuitakia mafanikio serikali mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako