• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi ya Uhuru Kenyatta inaelekea wapi?

    (GMT+08:00) 2014-10-08 10:59:57

    Intro: Rais Uhuru Kenyatta leo anahuhdhuria mkutano unaohusu kesi yake kwenye wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC mjini The Hague. Kumekuwa na maswali kuhusu rais Kenyatta kwenda mahakamani akiwa madarakani, na zaidi kutakiwa kuwepo mahakamani mwenyewe bila kuwakilishwa, matukio haya mawili yana maana gani na mwelekeo kesi inayomkabili. Mwandishi wetu Xie Yi ana zaidi.

    Reporter: Baada ya bunge la Kenya kushindwa kuchunguza machafuko baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, kesi hiyo iliwasilishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC mjini The Hague. Baada ya uchunguzi uliofanywa na mahakama hiyo, rais Kenyatta na maaofisa wengine kadhaa wa ngazi ya juu wa Kenya walifunguliwa mashtaka kwa mauaji na tuhuma nyingine za kukiuka ubinadamu. Rais Kenyatta alikana tuhuma dhidi yake. Kwenye mkutano wa leo, rais huyo ataitetea serikali yake inayolaumiwa kwa kuzuia idara ya kuendesha mashtaka kufanya uchunguzi na kukusanya ushahidi.

    Akizungumzia sababu ya kesi hiyo kuwasilishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, mchambuzi wa siasa nchini Kenya Bw Stephen Ndegwa amesema bunge la Kenya na idara nyingine huru hazina uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi kuhusu kesi hiyo, lakini ICC inadhaniwa kuwa na uwezo huo. Aidha, wabunge wengine na mashirika mengine ya kijamii nchini Kenya yaliitaka kesi hiyo iwasilishwe ICC, na baadhi ya nchi za magharibi zilishinikizo kesi hiyo iwasilishwe ICC.

    Rais Kenyatta aliwahi kuhudhuria mikutano ya ICC kabla ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchi. Lakini kwa sasa akiwa rais anakabiliwa na hali ngumu. Mtaalamu wa uhusiano wa kimataifa kutoka chuo kikuu cha kimataifa cha Marekani kilicho mjini Nairobi Muni Manchaya, amesema kwa upande mmoja Umoja wa Afrika unataka Kenyatta asiende ICC, na kwa upande mwingine akiwa rais wa Kenya, nchi ambayo ilisaini mkataba wa Rome, ana wajibu wa kuitikia mashtaka ya ICC. Ndiyo maana rais huyo ameamua kukabidhi madaraka kwa naibu wake Bw William Ruto na kwenda ICC mwenyewe, ili kuepusha ICC kutoa kibali cha kukamatwa kwake.

    Akizungumzia mwelekeo wa kesi hiyo, msemaji wa ICC Fadi el-Abdullah amesema, kuhudhuria mkutano wa ICC kwa Bw. Kenyatta kumeonesha moyo wake wa ushirikiano, na kama anafuata sheria husika ICC haitamshikilia.

    Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka chuo cha diplomasia na uhusiano wa kimataifa katika chuo kikuu cha Nairobi Matin Nguru, waendesha mashitaka wa ICC hawana ushahidi wazi wa kuhusika kwa rais Kenyatta katika machafuko baada ya uchaguzi, hali ambayo ni kikwazo kikubwa kwa kesi hiyo. Profesa Nguru anasema kesi hiyo itaendelea kufuatiliwa. Waendesha mashitaka wa kesi hiyo pia wamekiri kwamba, ushahidi uliopo haitoshi, wakati uchunguzi wa kesi hiyo unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako