• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Yang Jiechi afanya mazungumzo na Bw. John Kerry

    (GMT+08:00) 2014-10-19 19:30:42

    Mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi jana huko Washington amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. John Kerry, na kubadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa na nchi hizo mbili.

    Bw. Yang Jiechi amesema, China inamkaribisha rais Barack Obama wa Marekani kuhudhuria mkutano wa APEC na kufanya ziara nchini China, na kuongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Marekani kufanikisha mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili na kusukuma mbele zaidi ujenzi wa uhusiano wa aina mpya kati ya China na Marekani.

    Kwa upande wake, Bw. Kerry amesema rais Obama anatilia maanani ziara yake nchini China mwezi ujao, na anapenda kutumia fursa hiyo muhimu kujadiliana na rais Xi Jinping wa China kuhusu haja ya kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na China. Marekani inapenda kufanya juhudi pamoja na China ili kufanikisha mkutano wa APEC utakaofanyika mwezi ujao mjini Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako