• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka 2014 wa mawasiliano ya kitaaluma kuhusu ugonjwa wa UKIMWI wafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2014-10-20 18:06:05

    Mkutano wa mwaka 2014 wa mawasiliano ya kitaaluma kuhusu ugonjwa wa UKIMWI umefanyika leo hapa Beijing na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 1,000 kutoka China na nchi za nje. Wajumbe wa mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na Shirika la kinga na tiba ya magonjwa ya zinaa na Ukimwi la China watafanya mawasiliano na majadiliano kuhusu kinga na tiba ya UKIMWI.

    Mke wa rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni balozi wa Shirika la Afya Duniani kuhusu kinga na tiba ya kifua kikuu na UKIMWI, Bibi Peng Liyuan amehudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutoa tuzo ya kumbukumbu kwa wanasayansi wa nchi za nje waliotoa mchango mkubwa katika kinga na tiba ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako