• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano kati ya marais wa China na Marekani utahimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2014-10-20 18:35:13

    Rais Barack Obama wa Marekani atahudhuria mkutano usio wa rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa uchumi ya Asia na Pasifiki APEC utakaofanyika mwezi ujao hapa China. Rais Obama pia atafanya ziara nchini China, na kukutana na rais Xi Jinping wa China.

    Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai jana huko Washington amesema, mambo muhimu yatakayozungumzwa kwenye mkutano wa marais hao ni kuhimiza uhusiano wa aina mpya kati ya nchi hizo mbili uwe wa kina, halisi, na wa uaminifu. Chini ya mwelekeo huo, China na Marekani zitajadiliana na kushirikiana kuhusu masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, maambukizi ya Ebola, mapambano dhidi ya ugaidi, kuzuia kuenea kwa silaha za maangamizi, nishati safi, nishati endelevu, na mkataba wa uwekezaji wa pande mbili, pamoja na masuala mengine ya kimataifa, kikanda na yanayofuatiliwa na pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako