• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima kufaidika na mikopo.

    (GMT+08:00) 2014-10-20 18:52:25

    Wakulima nchini Uganda wanatarajiwa kufaidika na mpango mpya wa serikali ya nchi hiyo ya kuwapa mikopo yenye riba ya chini.

    Serikali ya nchi hiyo inasema inatarajia kutumia shilingi bilioni 60 ambazo imepata kutoka katika shirika la mfuko wa kilimo ulimwenguni IFAD.

    Fedha hizo kulingana na serikali ni kwamba zitakuwa zikipewa wakulima walio katika vikundi kama mkopo, na wanatarajiwa kuzitumia kuimarisha kilimo chao pamoja na ufugaji.

    Aidha serikali inasema inatarajia wakulima kuwa na mipango kabambe ya kufanyia fedha hizo, ili kuona kwamba zinawafaidi katika kilimo chao.

    Wakulima nchini humo wamekuwa wakilalama kutokana na riba za juu zinazitozwa na benki katika mikopo ambayo, wanalazimika kuchukua benki kuendeleza kilimo chao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako