• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mustakabali wa uchumi wa China bado ni mzuri ingawa unakabiliwa na hatari

    (GMT+08:00) 2014-10-22 11:17:33

    Mwanauchumi mkuu wa Benki ya Dunia ambaye pia ni naibu mkuu wa Benki hiyo Bw. Kaushik Basu hivi karibuni amesema, uchumi wa dunia ulifufuka kwa muda mfupi mwaka jana, lakini hivi karibuni umekabiliwa na baadhi ya matatizo, na huenda utadidimia tena. Wakati huo huo, ingawa kasi ya ongezeko la uchumi wa China imepungua, lakini bado iko mbele katika makundi makuu ya uchumi duniani.

    Bw. Basu amesema, miezi sita kabla wanauchumi wengi walidhani kuwa uchumi wa dunia utaongezeka kwa kiasi kikubwa, lakini takwimu za miezi kadhaa iliyopita zinaonesha kuwa, uchumi wa dunia unakabiliwa na hatari nyingi kwa mara nyingine.

    Bw. Basu amesema kasi ya ongezeko la uchumi wa Marekani imezidi asilimia 2, na idadi ya watu wanaopoteza ajira pia imepungua kwa kiasi kikubwa, lakini idadi ya watu wasio na ajira kwa muda mrefu bado ni kubwa, na hii ni hatari moja inayoukabili uchumi wa Marekani. Ulaya na Japan nazo zinakubwa na kudidimia kwa uchumi, na uchumi wa eneo linalotumia Euro haukuongezeka katika robo ya pili ya mwaka, na Japan pia.

    Bw. Basu amesema ingawa Marekani bado ni nguvu muhimu ya kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia, lakini katika miaka 15 hadi 20 ijayo, makundi yanayojitokeza kiuchumi zikiwemo China na India yatakuwa nguvu kuu ya kuhimiza ongezeko la uchumi.

    Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia inaonyesha kuwa benki hiyo imepunguza makadiro ya ongezeko la uchumi wa China kutoka asilimia 7.6 hadi 7.4, lakini imesisitiza kuwa, hatua za mageuzi zilizochukuliwa na serikali ya China zitafanya uchumi wa China uwe kwenye njia ya maendeleo endelevu. Bw. Basu amesema asilimia 7.4 ni ni ya kasi sana duniani.

    Bw. Basu amesema katika muda mfupi ujao uchumi wa China utakabiliwa na baadhi ya hatari, mojawapo ikiwa ni uwekezaji unaozidi kiasi kinachotakiwa, lakini mustakabali wa uchumi wa China bado ni mzuri sana.

    Amesema uwekezaji mwafaka unasaidia kuhimiza ongezeko la uchumi, na ongezeko la uwekezaji nchini China hapo awali limehimiza sana ongezeko la uchumi wa China na dunia. Lakini hivi sasa uwekezaji umechukua asilimia 50 hivi katika uchumi wa dunia, uwekezaji unaozidi kiasi mwafaka umepunguza faida za uwekezaji, na kama hali hiyo itaendelea, sekta ya fedha nchini China itakabiliwa na hatari kubwa.

    Wakati huo huo, Bw. Basu amesema serikali ya China imetambua hatari hiyo, na mageuzi ya muundo wa uchumi yanayofanyika nchini China yanaweza kutatua masuala hayo hatua kwa hatua, ingawa katika mchakato wa mageuzi hayo China itakabiliwa na matatizo mengi.

    Ameona kuwa China imeanza kupata mafanikio katika mageuzi ya miundo ya uchumi. Kutokana na kuinuka kwa gharama za nguvu kazi, hadhi ya sekta ya utengenezaji kwenye uchumi wa China imepungua pole pole, na hadhi ya sekta ya huduma imeinuka hatua kwa hatua. Hali hiyo inasaidia China kurekebisha miundo ya uchumi.

    Mwanauchumi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bw. Olivier Blanchard hivi karibuni amesema, kupungua kwa kasi ya ongezeko la uchumi wa China kunaonesha kuwa uchumi wa China unaendelezwa kwa njia safi. Amesema kuwa hatari kutoka sekta ya ujenzi wa nyumba na benki inaweza kudhibitiwa, lakini kuongezeka kwa uwekezaji huenda kutazuia marekebisho ya muundo wa uchumi nchini humo.

    Bw. Blanchard amesema, IMF imekadiria kuwa, hivi sasa ongezeko la uchumi wa China linaweza kufikia asilimia 7 hadi 8, lakini katika siku za baadaye kiwango cha asilmia 6 pia kitakubalika.

    Bw. Blandchard amesema, uchumi wa China unaendelezwa kama unakimbia mashindano ya mbio ndefu, na kama ongezeko la uchumi wa China likidumu kwa asilimia 10 kila mwaka, masuala mfululizo kama uchafuzi wa mazingira na upungufu wa rasilimali mijini yatatokea, hivyo China inalazimika kupunguza kasi ya ongezeko la uchumi. Ameongeza kuwa hata ongezeko la asilmia 6 pia ni kiwango kizuri.

    Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na IMF kuhusu matarajio ya uchumi wa dunia inakadiria kuwa, ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu na kwa mwaka ujao litafikia asilimia 7.4 na asilmia 7.1, ambapo makadirio hayo ni sawa na makadiro yaliyotolewa na shirika hilo mwezi Julai. Bw. Blanchard amesema, IMF imedumisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa China, kwani lina imani kuwa, hatari kutoka sekta ya ujenzi wa nyumba na (taasisi za fedha zisizo rasmi)? benki kivuli zinaweza kudhibitiwa.

    Bw. Blanchard amesema bei ya nyumba nchini China inaweza kupungua, lakini haitaleta hatari katika mambo ya kifedha, kwani familia na benki za China haziwezi kuvunjika kutokana na kupungua kwa bei ya nyumba. Ameona kuwa benki za kivuli zitaleta matatizo kwa mfumo wa fedha wa China, lakini serikali ya China ina uwezo wa kutosha wa kutoa msaada kama matatizo yoyote yatatokea.

    Bw. Blanchard amesema, China bado inakabiliana na changamoto nyingi katika mchakato wa marekebisho ya muundo wa uchumi. Hivi sasa kutegemea usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi inapungua, lakini kuongezeka sana kwa uwekezaji huenda kutazuia mchakato wa marekebisho ya muundo wa uchumi nchini China.

    Bw. Blanchard amesema athari iliyoletwa na msukosuko wa fedha duniani ni mbaya zaidi kuliko msukosuko wa uchumi wa karne iliyopita, na uchumi wa dunia unahitaji muda mrefu zaidi ili kufufuka tena. Anakadiria kuwa ongezeko la uchumi wa dunia halitafikia kiwango cha kawaida kabla ya mwaka 2016. Amesema sera ya fedha si njia ya ajabu inayohimiza ongezeko la uchumi, bali ni sehemu moja tu ya mpango kamili wa kuhimiza ongezeko la uchumi, na kuinua tija ya kazi ni njia ya kimsingi ya kuongezeka kwa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako