• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikwete asema China imetoa mfano wa mafanikio kwa Tanzania katika kufanikisha mageuzi ya kilimo

    (GMT+08:00) 2014-10-24 11:08:00

     

     

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania jana alitembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, na kutunukiwa uprofesa wa heshima wa chuo kikuu hicho na kutoa hotuba.

    Katika hotuba aliyoitoa kwa muda wa saa moja, rais Kikwete amesema haiwezekani kuzungumzia maendeleo ya Afrika bila kutaja kilimo, na katika nchi nyingi za Afrika, kilimo ni ni uti wa mgongo wa uchumi na theluthi mbili ya Waafrika wanategemea kilimo. Rais Kikwete pia alitaja "mageuzi ya kilimo" mara nyingi katika hotuba yake, na anaona kuwa China imetoa mfano wa mafanikio kwa Tanzania katika kufanikisha mageuzi ya kilimo. Anasema,

    "Mageuzi ya kilimo yamechukua nafasi kubwa katika kutimiza maendeleo ya kasi ya uchumi na lengo la kupunguza umaskini kwa muda mrefu nchini China. Kutokana na mapinduzi ya kilimo, China imefanikiwa kuongeza uzalishaji wa kilimo. Mafanikio iliyopata China katika kilimo yameipatia China faida kubwa, ikiwemo maendeleo ya uchumi na viwanda.

    Kikiwa mzizi wa elimu ya kupanda mbegu ya kisasa ya China, Chuo Kikuu cha Kilimo cha China chenye historia ya miaka karibu 100 kimeandaa wataalamu na wasomi wengi wa kilimo, na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo na mageuzi ya kilimo cha China. Katika miaka ya hivi karibuni, chuo kikuu hicho kimekuwa kinafanya juhudi kuandaa wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kilimo, mbali na kutatua tatizo la upungufu wa chakula la China, pia kimejitahidi kutoa mchango kwa neema ya watu wa nchi mbalimbali. Tanzania ni mwenzi muhimu wa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China.

    Kutokana na msaada wa Benki ya Dunia na Kituo cha Kimataifa cha kupunguza umaskini cha China, mkuu wa kitivo cha utamaduni wa binadamu na maendeleo katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Li Xiaoyun ambaye kwa miaka mingi amejihusisha katika kuisaidia Tanzania kuendeleza kilimo na kutimiza lengo la kupunguza umaskini, aliwahi kwenda Tanzania mara nyingi kufanya utafiti juu ya hali na masuala ya kilimo nchini humo. Profesa Li Xiaoyun anasema kutokana na utekelezaji wa sera ya Kilimo Kwanza na mpango wa maendeleo ya sehemu za vijijini, katika miaka ya hivi karibuni kiwango cha ongezeko la uzalishaji wa kilimo nchini Tanzania kimefikia asilimia 3.2 hadi 3.5, na tatizo la njaa nchini Tanzania halipo kabisa, uwiano kati ya uzalishaji wa nafaka na mahitaji umefikia asilimia 102, na uzalishaji wa ziada umetokea. Hata hivyo, Profesa Li Xiaoyun ametaja suala kuu linalokikabili kilimo cha Tanzania, yaani "ongezeko la uzalishaji wa kilimo halisaidii kupunguza umaskini".

    Anasema, "Kama zilivyo nchi nyingine za Afrika, kilimo cha Tanzania kinakabiliwa na suala kwamba kuna ongezeko lakini halijafanya kazi sana katika kupunguza umaskini. Ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania linafikia asilimia 3, na ongezeko la uzalishaji wa kilimo ni asilimia 3.2 hadi 3.5, ni juu kidogo tu kuliko ongezeko la idadi ya watu. Kilimo cha Tanzania ni cha kujikimu tu kwa chakula, na hakijaingia kipindi cha kusaidia kuhimiza maendeleo ya viwanda na mageuzi ya uchumi."

    Hivi sasa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China kinafanya ushirikiano na Tanzania katika kilimo kwa njia tatu. Kwanza ni kutoa ushauri wa kupanda, kupitia kuandaa makongamano na mawasiliano ya kielimu, chuo hicho kimewajulisha maofisa wa serikali ya Tanzania na wakulima uzoefu wa kilimo ulionao China. Pili ni kuwaandaa wataalamu wa kilimo, kuwaalika watu husika wa kilimo wa Tanzania kuja China na kupewa mafunzo. Tatu ni kutoa mfano wa moja kwa moja. Katika kijiji cha Peapea mkoani Morogoro, kituo cha kwanza cha kupunguza umaskini cha ngazi ya kijiji barani Afrika kimejengwa, ambako njia yenye umaalumu wa Kichina wa kukidhi mahitaji ya kijiji chote na ukoo wote imechukuliwa, na kuwafundisha mikono kwa mikono wakulima wa huko jinsi ya kutumia vizuri ardhi, kupalilia mashamba na kupanda. Katika miaka mitatu iliyopita tangu kituo hicho kianzishwe, uzalishaji wa mahindi katika kijiji hicho umeongezeka mara tatu.

    Rais Kikwete amekishukuru Chuo Kikuu cha Kilimo cha China kwa kusaidia Tanzania kuendeleza kilimo. Anasema hakika kituo cha kupunguza umaskini cha ngazi ya kijiji mkoani Morogoro kinasaidia nchi mbili za Tanzania na China kutimiza manufaa kwa pande mbili.

    Anasema, "nafahamu kuwa nyinyi mmejenga kituo cha mfano cha kilimo mkoani Morogoro, hiki ndicho tunachohitaji. Kwani mnaweza kufanya matokeo ya utafiti wenu kutumiwa katika mchakato wa uzalishaji halisi kwa wakulima wa Tanzania. Nakuhakikishia kwamba serikali ya Tanzania inaunga mkono kithabiti mpango huo. Nawashukuru kwa msaada wenu wa dhati kwa mageuzi ya kilimo nchini Tanzania."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako