• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wapongeza lengo la Umoja wa Ulaya la kupunguza utoaji wa hewa chafu

    (GMT+08:00) 2014-10-24 18:28:42

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza uamuzi wa viongozi wa Umoja wa Ulaya wa kupunguza utoaji wa hewa chafu inayotokana na mimea kwa asilimia 40 itakapofika mwaka 2030 ikilinganishwa na vigezo vya mwaka 1990.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu imesema, uamuzi huo unaonyesha mwendelezo wa uongozi wa Umoja wa Ulaya katika kuchukua hatua thabiti za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Taarifa hiyo imesema, kwa mara nyingine tena, bara la Ulaya linaongoza kwa juhudi zake za kutimiza malengo ya kupunguza utoaji wa hewa chafu.

    Rais wa Baraza la Ulaya Herman Van Rompuy amesema kuwa, makubaliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yatakuwa ni faraja ya kipekee kwake na kwa mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barosso, ambao wanamaliza muda wao wa uongozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako