• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampala Uganda:Shilingi ya Uganda yaendelea kudorora

    (GMT+08:00) 2014-10-24 19:55:34

    Benki kuu ya Uganda imeonywa kuwa ukosefu wa thamani ya shilingi ya nchi hiyo itasababisha mfumko mbaya wa uchumi.

    Wataalamu wa masuala ya uchumi nchini humo wameitaka benki hiyo kutafuta suluhisho la kupunguza mporomoko wa sarafu.

    Uganda sasa imekumbwa na ukosefu wa usawa wa biashara kutokana na tofauti kubwa kati ya shilingi yao na pesa za kigeni.

    Wafanyibiashara wa kimataifa nchini Uganda wameathirika pakubwa na hali hiyo inayoongeza gharama za biashara zao.

    Hii leo Dola moja ya Marekani imeuza kwa shilingi 2750 kutoka 2600 wiki iliyopita.

    Mwezi Septemba mfumko wa Uganda uliongezeka kwa asilimia 1.4

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako