• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa shehena ya nne ya msaada kwa nchi za Afrika magharibi kwa ajili ya kupambana na Ebola

    (GMT+08:00) 2014-10-24 20:21:23

    Rais Xi Jinping wa China leo ametangaza kuwa China itatoa shehena ya nne ya msaada kwa nchi za Afrika magharibi kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya Ebola.

    Rais Xi amesema, kutokana na maendeleo ya maambukizi ya Ebola na mahitaji ya nchi zilizoathiriwa na ugonjwa huo, serikali ya China imeamua kutoa shehena ya nne ya misaada ya vifaa na fedha yenye thamani ya yuan milioni 500 kwa nchi tatu za Liberia, Sierra leone na Guinea pamoja na mashiriki husika ya kimataifa. Ameongeza kuwa China itatuma zaidi wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza na madaktari katika nchi hizo na kujenga kituo kimoja cha huduma za matibabu nchini Liberia. China pia inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kuzisaidia nchi zilizoathirika na Ebola kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.

    Rais Xi ametangaza uamuzi huo alipokutana na rais Jakaya Kiwete wa Tanzania ambaye yuko ziarani nchini China. Spika wa Bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang pia amekutana kwa nyakati tofauti na rais Kiwete.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako