• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Mali aaga dunia

    (GMT+08:00) 2014-10-25 19:45:00

    Mali imetangaza tukio la kwanza la maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini humo baada ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 2 kufariki kwa ugonjwa huo.Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Hospitali ya Kayes magharibi ya Mali Daktari Toumani Konare, jumla ya watu 23 wamewekwa chini ya karantini wakiwemo watu 12 wa familia ya msichana huyo pamoja na maofisa 11 wa matibabu. Habari nyingine zinasema, msaidizi wa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Marie Paule Gini amesema, zaidi ya chanjo elfu 10 za Ebola zinatarajiwa kuanza kutumiwa rasmi mapema mwa ujao. Pia amesema, kama matokeo ya majaribio ya awali yatakuwa mazuri, basi madaktari, wauguzi na watu wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo Afrika Magharibi watapatiwa chanjo hiyo Desemba mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako