• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Kikwete atembelea mkoa wa Shandong,China

    (GMT+08:00) 2014-10-25 20:33:21

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania leo aliendelea na ziara yake ya siku sita nchini China kwa kutembelea mkoa wa Shandong. Katika mkoa wa Shandong, rais Kikwete alifanya mazungumzo na katibu wa kamati ya chama cha kikomunisti mkoani Shandong Bw Jiang Yikang ambaye alimfahamisha kuhusu maendeleo ya mkoa huo na hali ya ushirikiano kati ya mkoa huo wa Shandong na Tanzania. Kwa upande wake, rais Kikwete amepongeza maendeleo ya yaliyopatikana katika mkoa huo na kuongeza kuwa Tanzania na Shandong zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu haswa katika sekta ya afya tokea mwaka wa 1968. Amesema tangu mwaka wa 1968, mkoa wa Shandong umetuma timu 23 za madaktari na zaidi ya maofisa wa matibabu 1,700 wamefanya kazi nchini Tanzania. Kikwete aliomba mamlaka ya mkoa huo kuongeza idadi ya madaktari wanaotumwa nchini Tanzania.Kikwete pia alitembelea kituo cha mafunzo ya kijeshi ambako alikutana na baadhi ya wanajeshi wa China ambao waliwahi kufanya kazi nchini Tanzania na kubadilishana maoni na wenyeji wa Shandong kuhusu ushirikiano wa kijeshi kati ya China na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako