• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chanjo ya Ebola yaanza kufanyiwa majaribio nchini Usiwisi wiki hii

    (GMT+08:00) 2014-10-29 19:14:33

    Hatimaye chanjo ya Ebola inayosubiriwa kwa muda mrefu inaanza kufanyiwa majaribio wiki hii nchini Uswisi.

    Mwandishi wetu Pili analeta zaidi.

    Shirika la afya duniani WHO linasimamia majaribio hayo.

    Msemaji wa shirika hilo Tarik Jasarevic anasema:

    "Kibali hiki kinamaanisha kuwa watu wapatao 120 waliojitolea mjini Lausanne watatumika katika majaribio ya chanjo hizi. Majaribio haya pia yanaendelea nchini Mali, Uingereza na Marekani. Chanjo hii inatokana na virusi vya aina moja kutoka sokwe ambayo jeni yake imebadilishwa."

    Watu hao waliojitolea watasimamiwa kwa miezi sita ili kuthamini usalama na ufanisi wa chanjo hiyo.

    Wakati huohuo, Australia imetangaza kuwazuia watu kutoka nchi za Afrika magharibi zinazoathirika na Ebola kuingia nchini humo.

    Waziri wa uhamiaji wa Australia Scott Morrison amesema

    "Hatua hizi ni pamoja na kusimamisha kwa muda mradi wetu wa uhamiaji, ukiwemo mradi wa kibinadamu na nchi zenye maambukizi ya Ebola, hatua hii inamaanisha kwamba hatushughulikii ombi lolote kutoka nchi zilizoathirika na ugonjwa huu."

    Uamuzi huo wa Australia umelaaniwa na nchi za Afrika Magharibi zinazoathirika na ugonjwa huo, zikisema ni uonevu kwa watu wenye afya nzuri na inaweza kuleta ugumu katika mapambano dhidi ya Ebola.

    Hatua hiyo ya Australia inafuatia uamuzi uliotolewa na Marekani kuhusu kuwaweka karantini wanajeshi wake waliorudi kutoka Italia, ambapo wanatoa msaada wa kuzuia Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako