• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa asema, mkutano wa kimataifa ni muhimu kwa ujenzi wa maafikiano nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2014-10-30 19:16:38

    Mkutano wa nne wa ngazi ya mawaziri kuhusu Afghanistan wenye kauli mbiu "Kuongeza ushirikiano kwa usalama endelevu na mafanikio ya kanda ya Asia" utakaofanyika kesho hapa China ni muhimu kwa ujenzi wa maafikiano kati ya nchi muhimu za Asia.

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Liu Jieyi amesema, mkutano huo si tu ni wa kwanza wa kimataifa kuhusu Afghanistan kufayika nchini China, bali pia ni mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu Afghanistan utakaofanyika baada ya kuundwa kwa serikali mpya nchini humo mwishoni mwa mwezi uliopita.

    Liu amesema mkutano huo ni wa pekee wa kikanda kuhusu Afghanistan unaoongozwa na nchi muhimu za muhimu la Asia, na unafuata kanuni za uongozi wa kikanda, umiliki, na maafikiano.

    Inafahamika kuwa waziri mkuu wa China Li Keqiang na rais Ashraf Ghani wa Afghanistan watahudhuria na kuhutubia hafla ya kuanza kwa mkutano huo.

    Mkutano huo pia utahudhuriwa na ujumbe wa Marekani utakaoongozwa na mshauri wa rais Barack Obama John Podesta na kuwashirikisha maofisa waandamizi kutoka kamati ya usalama wa taifa, wizara ya mambo ya nje na shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani.

    Mkutano huo utafanyika wakati wa ziara ya rais Ghani nchini China. Rais huyo mpya wa Afghanistan ameichagua China kuwa nchi ya kwanza ya kutembelea baada ya kuingia madarakani mwezi uliopita. Akitoa hotuba kwenye chuo kikuu cha Tsinghua hapa Beijing rais Ghani ameitaja China kama mwenzi wa kimkakati wa nchi yake. Wachambuzi wengine wa siasa nchini Afghanistan pia wanaona, China ikiwa ni uchumi mkubwa wa pili duniani na jirani mwema wa Afghanistan, inaweza kuwa na kazi muhimu ya kufanya katika kuleta utulivu nchini Afghanistan kupitia uwekezaji na kuishawishi Pakistan kuacha eti uungaji mkono kwa kundi la Taliban, kauli ambayo imekanushwa na upande wa Pakistan.

    Tangu mwaka 2002, China imechangia mamilioni ya dola za kimarekani kwa mchakato wa ukarabati wa Afghanistan. Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyosainiwa wakati wa ziara ya rais Ghani nchini China, China itatoa ufadhili wa dola zaidi ya milioni 80 kwa serikali ya Afghanistan kwa mwaka huu na dola nyingine milioni 240 katika miaka mitatu ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako