• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gharama vifaa vya ujenzi mtihani kwa NSSF

    (GMT+08:00) 2014-10-30 20:13:59

    Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeiomba Serikali kusaidia kuzuia kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi ili kuruhusu miradi mikubwa inayotekelezwa na mfuko huo imalizike kwa wakati.

    Ombi hilo lilitolewa kwa Kamati ya Bunge ya Ustawi wa Jamii ilipotembelea miradi ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni, nyumba za makazi za Kijichi na mradi wa kijiji cha kisasa cha Dege huko Kigamboni.

    Akitoa maelezo kwa kamati hiyo kuhusu maendeleo ya miradi hiyo, Meneja wa Miradi ya NSSF, Mhandisi John Msemo anasema ujenzi wa daraja la Kigamboni unaendelea vizuri na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani, badala ya Januari kama ilivyopangwa awali.

    Shirika hilo la serikali linamatarajio kama hakutakuwa na matatizo ya upandaji wa bei ya malighafi za ujenzi, miradi hiyo itakamilika kwa wakati Na pia wanaiomba Serikali iwasaidia.

    Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi wa Jamii, Saidi Mtanda (Mchinga) alisema kamati yake imeridhika na maendeleo ya miradi hiyo mikubwa ambayo ni mfano wa kuigwa na wtapeleka maombi yao serikalini ili kuangalia namna ya kusaidia upugunguzwaji wa gharama hizo za vifaa.

    Mkurugenzi wa NSSF, Dk Ramadhan Dau alisema kutokana na kasi ya miradi hiyo na mabadiliko yanayoonekana, wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kununua nyumba za kisasa zilizopo kwenye miradi hiyo ya Dege na Kijichi ili kupata makazi bora na ya kisasa kwa gharama nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako