• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uamuzi uliotolewa na mkutano wa kamati kuu ya CPC waonesha nia imara ya chama kutawala kwa mujibu wa sheria

    (GMT+08:00) 2014-10-31 09:32:03

    Vyombo mbalimbali vya habari vimetoa maoni kuhusu uamuzi uliotolewa kwenye mkutano wa nne wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kuhimiza kikamilifu utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria, na kuona uamuzi huo umeonesha nia imara ya Chama cha kikomunisti cha China katika kuhimiza utawala wa kisheria.

    Shirika la habari la Bloomberg la Marekani limesema uamuzi huo umeonesha juhudi mpya za Chama cha Kikomunisti cha China katika kurekebisha mfumo wa sheria na kuongeza nguvu ya kupambana na ufisadi.

    Shirika la habari la Korea limetoa tahariri likisema hatua zilizotangazwa kwenye mkutano huo zikiwemo kuamua siku ya katiba na kujenga utaratibu wa kuapisha wa katiba zitaongeza kwa kiasi kikubwa mwamko wa watu kuhusu sheria.

    Gazeti la Zaobao la Singapore limesema uamuzi huo si tu umeweka mipaka ya madaraka ya maofisa na kuhimiza haki kwenye sheria, bali pia umeonesha ujasiri wa chama cha Kikomunisti cha China katika kuhimiza mageuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako