• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Burkina Faso atangaza hali ya hatari

    (GMT+08:00) 2014-10-31 10:18:11

    Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso ametangaza hali ya hatari baada ya wananchi kufanya maandamano ya vurugu kupinga mwito wa serikali kuwataka wabunge wafanye marekebisho ya katiba, kumruhusu Rais Compaore aendelee kuwa madarakani baada ya kipindi chake cha pili kwisha mwezi Novemba mwaka kesho kwa mujibu wa katiba. Bwana Compaore amekuwa madarakani kwa miaka 27.

    Habari zinasema jeshi la nchi limetwaa udhibiti wa nchi na kutangaza kuvunja bunge na serikali, na kuunda chombo cha mpito. Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Nabere Honore Traore amesema chombo hicho cha mpito kitawekwa madarakani kwa mashauriano na vyama vyote.

    Jumuiya ya kimataifa imeonesha kuwa na wasiwasi na hali inayoendelea nchini Burkina Faso. Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi Nkosozana Dlamini Zuma amesema ameshitushwa na hali nchini humo na kutaka pande zote zijizuie. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Ban Ki Moon pia amesema ana wasiwasi na maendeleo ya hali nchini Burkina Faso na amemtaka mwakilishi wake maalumu kuhusu Afrika Magharibi Bw Mohamed Ibn Chambas kuangalia hali nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako