• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yamwita balozi wake kutoka Sweden

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:03:33

    Israel imemwita nyumbani balozi wake kutoka nchini Sweden kulalamikia hatua ya nchi hiyo ya kutambua taifa la Palestina. Duru zinaarifu kuwa balozi Yitzhak Bachman alirejea Israel kutoka Stockholm kwa mashauriano na serikali.

    Wizara ya mambo ya nje ya Israel itaamua kama itamrejesha balozi huyo au la na iwapo hatorejea basi hatua hiyo itaathiri vipi uhusiano wa kidiplomasia kati ya Sweden na Israel. Sweden imekuwa nchi ya kwanza ya magharibi kutambua taifa la Palestina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako