• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamishna wa polisi wa Somalia afariki Mogadishu

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:15:21

    Kamishna wa polisi wa Somalia jenerali Mohamed Sheik Hassan Ismael amefariki kwenye mji mkuu Mogadishu baada ya kupelekwa hospitali na wasaidizi wake.

    Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia alituma salamu za rambirambi kwa watu wa Somalia na kuamuru uchunguzi uanze mara moja kubaini kilichosababisha kifo chake.

    Ofisi ya waziri mkuu wa Somalia ilithibitisha kufariki kwa kamishna huyo na kuunda tume ya mawaziri watano ya kuchunguza kifo hicho cha ghafla.

    Duru za karibu na tume hiyo zimearifu kwamba mwili wa kamishna huyo utapelekwa kwenye hospitali moja ya Uturuki mjini Mogadishu kufanyiwa uchughuzi.

    Aidha watu kadhaa wakiwemo wahudumu wa hoteli alikokula chakula cha mchana kamishna huyo wamekamatwa na kuhojiwa kwenye idara ya kuchunguza uhalifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako