• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi wa China atoa mwito wa kuongeza ufanisi wa kampeni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:18:47

    Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wang Min amesema ni lazima kuongeza ufanisi wa kampeni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, na kutilia maanani kuimarisha ujenzi wa uwezo wa kulinda amani.

    Bw. Wang Min amesema China inaunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kuhusu kufanya tathmini kwa pande zote kampeni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, na kukubali kuboresha kazi katika sekta ya kulinda amani kwenye msingi wa kufikia maoni ya pamoja, na kupata maendeleo mwaka kesho wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

    Bw. Wang Min amesema China inaunga mkono kithabiti na kushiriki kwenye kampeni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa. Hivi sasa walinzi wa amani wa China karibu 2,200 wanatekeleza majukumu 9 ya kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mali na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako