• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam wa akiolojia kutoka Kenya asaidia wanafunzi wa China kufahamu zaidi historia ya china na Afrika mashariki.

    (GMT+08:00) 2014-11-05 09:25:25

    Dkt. Herman Kiriama ni mtaalam wa akiolojia kutoka kenya amealikwa kufunza historia ya uhusiano wa jadi wa China na Afrika Mashariki kwenye Chuo cha Peking mjini Beijing

    Huyu ni mfanya biashara wa kichina akiuza bidhaa mjini Mombasa pwani ya kenya-amejifunza lugha ya Kiswahili ambayo inazungumzwa na wengi mjini hapa ili kumwezesha kuwasiliana vyema na wateja wake.

    Yeye ni mfano tu wa idadi inayoendelea kuongezeka ya wachina wanaofika Afrika kufanya biashara.

    Siku hizi uwepo wa wachina barani Afrika na waafrika nchini China umekuwa ni jambo la kawaida kwenye macho ya wengi.

    Lakini kulingana na historia uhusiano huo umekuwepo kwa zaidi ya miaka 600 iliopita.

    Na bado wachina na wakaazi wengi wa Afrika mashariki hawajafahamu ushirikiano wa kibiashara wa tangu jadi kati ya kati ya pande zote mbili.

    Katika juhudi za kusaidia wanafunzi wa kizazi cha sasa kuelewa zaidi ushirikiano huo pamoja na historia yake, Chuo kikuu cha Peking mjini Beijing kimemwalika Dkt. Herman Kiriama kutoa mafunzo.

    …….Leo anafunza kuhusu mabaki ya vigae na vifaa vingine vya kichina ambavyo vimepatikana katika eneo la Malindi nchini Kenya.

    "Mafunzo kama haya ndio yatasaidia watu kujua na pia tuko kwenye harakati za kuandika vitabu za kuonyesha vile uhusiano ulivyokuwa kwa sababu watu wanajua tu kulikuwa na uhusiano lakini hawajui ulikuwa wa aina gani "

    Kulingana na historia mwaka wa 1418 wakati wa enzi ya Ming meli moja ya China inayomilikiwa na Zheng He ilifika mjini Malindi.

    Na mwaka uliopita mwana akiolojia Chapurukha Kusimba kutoka Marekani na wenzake kutoka Kenya walipata sarafu ya China katika kisiwa cha Manda kaunti ya Lamu.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako