• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya wastadi wa Kongfu China yafungua zaidi ufahamu wao kuhusu mchezo huo.

    (GMT+08:00) 2014-11-06 17:11:33

    Nchini Tanzania kuna zaidi ya vikundi 40 vya ustadi wa Kungfu.

    Lakini sio wote ambao wanafahamu vyema historia ya sanaa hiyo ya China kwani hawajahi kwenda nchini China.

    Ili kuwawezesha kupata ufahamu wa jumla wa mchezo huo, taasisi moja kutoka mkoa Henan nchini China iliwaalika wastadi wa kungfu kutoka Tanzania kutembelea China.

    Bi Yao Ting ni afisa kwenye taasisi hiyo ya Chanjiagou.

    "Tuliandaa darasa la kujifunza lugha na tamaduni za kichina..pia walifunzwa jinsi ya kucheza kungfu. Wasanii pia walitembelea katika mkoa wa Henan ambao una mahadhari mengi. Walitembelea eneo la Chanjiagou ambao ni chanzo cha kungfu ya taiji. Tulitaka washiriki wote kutoka Tanzania wapate ufahamu wa jumla kuhusu watu, lugha na tamaduni za kichina kwa sababu mara nyingi watu wanapokuja hapa wanaiuliza …mwalimu..ni kweli kwamba kila mchina anaweza kucheza kungufu? Lakini kwa hakika sio kweli"

    Walioshiriki ziara hii ni wachezaji wa kungufu kutoka zaidi ya vikundi 20 nchini Tanzania.

    Ndani ya wiki mbili walizokuwa China wameweza kunoa makali yao na wana matumaini ya kufanya vyema kwenye mashindano ya Wushu baina ya kimataifa mwaka ujao nchini Tanzania.

    Bwana Saleh Mwidini Mtaula ni katibu wa shirikisho la Kungfu nchini Tanzania.

    "Kuna mambo mengi ambayo tumejifunza hapa kama vile tamaduni za China. Pia tumejifunza kitu kama matumizi ya pombe. Wengi tulidhania kwamba pombe ni kwa ajili ya kunywa tu lakini kumbe ni sehemu ya utamaduni wa China na pia ina maadili mengi. Tumetembelea pia vyuo vya Wushu na tunadhani mashindano ya kimataifa ya mwaka ujao tutafanya vyema. "

    Kusoma lugha na tamaduni za kichina hakutaishia kwenye ziara hii mbali pia watakaporejea nyumbani wachezaji hawa wataendelea kujifunza kwenye taasisi za Confucius zilizoko nchini humo.

    Mfaume Saidi ni mchezaji wa Kungfu na anasimamia vikundi vitatu nchini Tanzania.

    Hii ni mara yake ya pili kuja nchini China.

    Mara ya kwanza alitembelea hekalu la Shaolin ambalo ni maarufu kwa ustadi wake wa Kungufu.

    "Nitakuwa na mipango mingi ya kuwafikisha wachezaji kwenye hatua ambayo ina mtazamo mzuri katika jamii kwa sababu kama wachezaji wa mchezo huu hawatakuwa na maisha mazuri basi inaweza kuleta picha kwamba hauna maana…kwa hivyo nitahakikisha kila mchezaji wa Wushu ana nafasi zuri na kujivunia kazi hiyo"

    Kama vile nchi nyingi za Afrika, idadi ya wachina wanaofika Tanzania kuwekeza ama kutekeleza miradi inaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.

    Ripoti ya shirika la Imara Group inaonyesha kwamba China imefungua zaidi ya nafasi 150, 000 za ajira kwa watanzania hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuliko wawekezaji wengine wa kigeni.

    Lakini mara kwa mara kukosa kufahamu lugha na tamaduni za pande zote mbili imekuwa ni changamoto ya kuwasiliana.

    Hadija Mcheka ni afisa wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini Tanzania na anahusika na kutathmini lugha zinazofaa kufunzwa shuleni.

    "Lugha yao ni zuri, sio ngumu sana kujifunza lakini tofauti kubwa na sisi ni vile wanavyotamka maneno. Nchini Tanzania kuna wachina wengi wameingia katika nyanja mbalimbali kama vile ufundi, biashara na kampuni nyingi za kichina na tunataka watanzania waingie kufanya kazi na wachina lakini pia tunataka wajifunze lugha kwa sababu hilo ndio tatizo tulilo nalo kwa sasa hivi"

    Na huku wachina na watanzania wakiendelea kutangamana zaidi, pia kuna haja ya kuongeza ufahamu wa lugha na tamaduni za pande zote mbili.

    Shirika la habari la TBC nchini Tanzania limekuwa ni mojawepo wa vyombo muhimu vya kuelimisha watu nchini huko kuhusu matukio ya china.

    Mwandishi wa habari za michezo Godffrey Nagwa kutoka TBC ameandamana na wachezaji Kungfu kwenye ziara hii ya China.

    "Nina imani kwamba kupitia vipindi vya michezo TBC kama vile michezo wiki hii na makala mbalimbali vitatoa taswira ya mchezo huu ndani ya Tanzania, Afrika Mashariki nap engine Afrika kwa ujumla "

    China ni yenye utamaduni mpana sio tu lugha na kungfu, lakini kujifunza mchezo huu ni hatua zuri ya kuelekea kufahamu desturi za China na watu wake.

    Wastadi wa kongfu kutoka Tanzania kwenye kasri la mfalme wa kale maarufu kama forbidden city ambalo sasa ni jumba la makumbusho lililoko mji mkuu Beijing. Ni baadhi ya maeneo waliotembelea baada ya mafunzo.

    Mwongozaji wa China atoa maelezo kuhusu sehemu watakazotembelea wastadi wa kongfu kutoka Tanzania. Wasatdi hao walitembelea maeneo mbalimbali nchini China baada ya kupata mafunzo.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako