• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatunga mpango wa kuendeleza miji ya Smart Cities katika siku zijazo

    (GMT+08:00) 2014-11-11 16:52:08

    Kongamano la tatu la ujenzi wa miji ya Smart Cities kati ya China na Ujerumani lililoandaliwa na taasisi ya uhandisi ya China, taasisi ya sayansi na uhandisi na Ujerumani na serikali ya mji wa Wuhan lilimalizika mwishoni mwa mwezi uliopita.

    Katika kongamano hilo la siku tatu, wataalamu, wanaviwanda, na maofisa wa serikali zaidi ya 200 walijadili ujenzi wa mji hiyo, kutafuta maendeleo endelevu ya miji, na kutunga mpango wa kuendeleza Smart Cities katika siku zijazo.

    Wataalamu walisema katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuharakishwa kwa maendeleo ya miji duniani, matatizo mbalimbali yametokea.

    Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa zaidi ya nusu ya watu wanaishi mijini, na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 asilimia 60 ya watu wataishi mijini. Idadi kubwa ya watu na msongamano barabarani umeathiri vibaya maisha ya watu, hivyo kuharakisha ujenzi wa miji aina ya Smart Cities kunaendana na mwelekeo wa maendeleo ya miji duniani.

    Mtaalamu mmoja wa taasisi ya sayansi na uhandisi ya Ujerumani alisema katika siku zijazo teknolojia mpya zitatumiwa katika kila jengo, kila gari na maisha ya kila mtu, teknolojia hizi zitaboresha mgawanyo wa rasilimali, kuongeza ufanisi kwenye jamii, na kujenga miji ambayo inafaa kwa maisha ya watu, kubana matumizi ya rasilimali, na kutokuwa na matatizo mengi.

    Mjumbe wa taasisi ya uhandisi ya China Bw. Pan Yunhe alisema, matumizi ya kompyuta na ujenzi wa mtandao wa Internet umeimarika mijini, na miji ya Smart Cities imejengwa kimsingi. Mwaka jana baraza la Atlantiki la Marekani lilitoa ripoti ya mwelekeo wa dunia likisema, mageuzi makubwa ya kiteknolojia yanatokea duniani, mageuzi hayo ni pamoja na utengenezaji kwa teknolojia mpya, nishati mpya na miji ya Smart Cities.

    Mkuu wa taasisi ya uhandisi ya China Bw. Zhou Ji inaona kuwa, ujenzi wa Smart Cities ni mwelekeo mpya wa miaka ya hivi karibuni. Jambo hili si kama tu linaweza kuhimiza uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, bali pia kusukuma mbele mageuzi na uboreshaji wa shughuli, kuboresha usimamizi wa miji, kuinua uwezo wa ushindani, na kuendesha miji kwa usalama na ufanisi zaidi.

    Kwenye hotuba yake, mjumbe kutoka Umoja wa Ulaya Prof. Phillip amesema ujenzi wa Smart Cities unahusisha mambo mengi, yakiwemo mawasiliano ya habari, maendeleo ya viwanda, mtandao wa Internet, utengenezaji kwa teknolojia mpya, usafiri, usambazaji wa vitu, mazingira ya miji, matibabu na usalama wa miji. Nchini China ujenga miji hiyo utafanyika zaidi katika mji yenye ukubwa wa kati, ambao utatatua matatizo ya idadi kubwa ya watu na msongamano barabarani.

    Bw. Pan Yunhe alisema serikali ya China inatilia mkazo ujenzi wa Smart Cities. Hivi sasa zaidi ya miji 300 imeweka kazi hii kwenye mpango wa 12 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi na jamii. Baadhi ya miji imetenga fedha nyingi zaidi kwa matumizi ya teknolojia mpya katika mambo ya usafiri na matibabu. China inajaribu kujenga miji mingi ya Smart Cities ifikapo 2020.

    Kwenye kongamano hilo, maofisa wa serikali kutoka miji ya Wuhan, Hangzhou na Dalian wamesema baadhi ya nchi ikiwemo Ujerumani zimetangulia katika ujenzi wa Smart Cities, na China itapenda kujifunza mawazo ya kisasa na uzoefu wa nchi hizo, ili kuinua uwezo wa kujenga na kusimamia miji na kutoa huduma mijini. Pia inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi hizi, ili kunufaika pamoja na fursa za maendeleo.

    Kuhusu suala la kulinda usalama wa habari kwenye mtandao wa Internet litakalotokea katika ujenzi wa Smart Cities, wataalamu wengi walipendekeza kuwa usanifu na utekelezaji wa mpango wa kujenga Smart Cities unahitaji kutilia mkazo kuzuia matishio mbalimbali, kuimarisha mfumo wa kulinda usalama wa habari kwenye mtandao wa Internet, na kuanzisha utaratibu wa kulinda habari kuhusu watu binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako