• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapata maendeleo makubwa katika masuala ya wanawake

    (GMT+08:00) 2014-11-06 20:19:35

    Mkuu wa idara ya kimataifa ya shirikisho la wanawake la China Bibi Mu Hong leo amesema, baada ya China mpya kuanzishwa, hasa katika miaka zaidi 30 iliyopita tangu China ifanye mageuzi na kutekeleza sera ya kufungua mlango, masuala yanayohusu wanawake nchini China yamepata maendeleo makubwa.

    Takwimu zinaonyesha kuwa, wanawake wamechukua asilimia 45 kati ya wachina milioni 770 wanaopata ajira, na hadi kufikia mwaka 2010, pengo la muda wa elimu kati ya wanawake na wanaume limepungua hadi mwaka 0.76.

    Bibi Mu Hong amesema, ingawa mafanikio yamepatikana, lakini China bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika maendeleo ya wanawake na kulinda haki na maslahi ya wanawake. Ametolea mfano ubaguzi wa kijinsia wakati wa kutafuta ajira, suala la kulinda haki na maslahi ya wanawake wanaofanya kazi za vibarua, biashara ya kuuza wanawake, na mabavu dhidi ya wanawake katika familia, na kusema serikali ya China na idara husika zimechukua hatua kukabiliana na masuala hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako