• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafugaji wa kabila la Watibet wanaohifadhi wanyama pori kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet

    (GMT+08:00) 2014-11-26 18:04:51

    Mfugaji Zangduo wa kabila la Watibet anasimama kando ya mto akiwa na dira na kalamu. Inaonekana kuwa Bw. Zangduo anatazama mteremko wa mlima wenye nyasi ndefu tu, lakini ukweli ni kwamba, anatazama makumi ya paa wanaotembea kwenye mteremko huo. Bw. Zangduo anawaangalia kwa makini kwa darubini, halafu anarekodi kwenye kitabu chake kwamba "saa tano na dakika 36 asubuhi, paa 40 wako mita 700 kaskazini mashariki ya kituo cha pili cha uangalizi".

    Bw. Zangduo mwenye umri wa miaka 30 ni mfugaji wa kawaida wa kijiji cha Yunta cha kata ya Haxiu mkoani Qinghai. Anaishi milimani tangu utotoni. Licha ya kuwa mfugaji, yeye pia ni mwangalizi wa kujitolea wa wanyama pori.

    Kutokana na mradi wa uchunguzi wa idadi ya wanayama pori wanaoishi katika eneo la chanzo cha mito mitatu ikiwemo mto Changjiang, mto manjano na mto Lancang, mwezi Novemba mwaka 2012 kata ya Haxiu na kituo cha uhifadhi wa mazingira cha Chuo Kikuu cha Peking vilitoa mafunzo ya uangalizi wa wanyama kwa wakazi wa huko. Wanakijiji 13 wa kijiji cha Yunta akiwemo Bw. Zangduo walipata mafunzo hayo na kuanza kuwaangalia paa kwa njia ya kisayansi.

    Kila mwezi Bw. Zangduo anatoka kijijini kwake kilichoko umbali wa mita 4200 kutoka usawa wa bahari na kwenda vituo vya uangalizi vyenye urefu wa mita 5000 kutoka usawa wa bahari. Anatakiwa kupiga picha na kurekodi kwenye vituo sita, kubadilisha SD kadi na betri za kamera zinazotumiwa kuangalia chui-theluji, na kurekodi vinyesi na nyayo za miguu za mbwa mwitu, dubu na chui-theluji.

    Bw. Zangduo anayeangalia paa tangu utotoni anajua vizuri tabia yao. Anasema, "Kila asubuhi paa wanakunywa maji bondeni, na mchana wanakula nyasi kwenye kilele cha mlima. Leo wamekwenda mlima mwingine, kwa sababu mbwa mwitu wamekuja." Akichukua fuvu la paa anasema, "Paa huyu alifariki akiwa na umri wa miaka minane na nusu. Angalia mistari kwenye pembe zake, mstari mmoja unamaanisha umri wa mwaka mmoja."

    Ingawa ameangalia paa kwa miaka mingi, lakini bado anafurahi sana kuwa mwangalizi wa kujitolea. Alisema anapenda wanyama pori, lakini zamani hakujua namna ya kuwahifadhi. Amejifunza njia nyingi za kisayansi za kuhifadhi wanyama pori kupitia mafunzo yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Peking, pia amepata vifaa mbalimbali.

    Waangalizi wa wanayama pori kama Bw. Zangduo ni muhimu sana kwa kazi ya uhifadhi wa mazingira katika eneo la chanzo cha mito mitatu. Eneo hili lina ukubwa wa zaidi ya kilomita laki 1.5 za mraba. Watafiti wachache hawawezi kumaliza kazi ya uangalizi. Ofisa wa mradi wa ukaguzi wa wanyama pori katika eneo la chanzo cha mito mitatu wa kituo cha uhifadhi wa mazingira cha Chuo Kikuu cha Peking Bw. Zhang Xiang alifahamisha kuwa, kijiji cha Yunta ni kijiji cha kwanza cha majaribio ya uangalizi wa paa. Wafugaji wa kijiji hiki wanaojitolea kuwaangalia wanyama pori wamekisaidia kituo hiki kupata habari mbalimbali kuhusu maisha ya paa, kutafiti uhusiano kati ya paa, chui-theluji na nzao wa manyoya marefu, na kutoa data mbalimbali kwa utungaji wa sera za kuhifadhi wanyama pori.

    Bw. Zhang alisema kuwahamasisha wafugaji kushiriki kwenye uchunguzi wa wanyama pori, si kama tu kutasaidia ukusanyaji wa data za wanyama pori, bali pia kutainua wazo la kuhifadhi mazingira la wafugaji.

    Baada ya kuwaangalia paa kwa siku moja, Bw. Zangduo alirudi nyumbani akichukua kitabu chenye rekodi nyingi na SD kadi ya kamera. Kutokana na kufanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu, Bw. Zangduo alipewa hati ya mwangalizi hodari wa kata ya Haxiu. Lakini moyoni mwake, jambo linaloweza kumfurahisha zaidi ni kuangalia paa na wanyama pori wengine kuishi kwa raha katika maskani yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako