• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa APEC wapitisha mpango wa uongozi wa eneo la biashara huria la Asia-Pasifiki

    (GMT+08:00) 2014-11-25 11:00:58

    Mkutano wa viongozi wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia Pasific APEC, umemalizika wiki iliyopita hapa Beijing. Mkutano huo ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 1500 wakiwemo viongozi na wajumbe wa makundi 21 ya uchumi ya jumuiya hiyo, viongozi wa sekta za viwanda na biashara wa kanda hiyo na wasomi maarufu. Washiriki hao walifikia maoni ya pamoja kuhusu kuzindua mchakato wa ujenzi wa eneo la biashara huria la Asia-Pasifiki, kuhimiza mawasiliano, na kutafuta maendeleo ya uvumbuzi.

    Kanda ya Asia-Pasific ina asilimia 40 ya idadi ya jumla ya watu duniani, na GDP yake ya jumla inachukua asilimia 60 ya ile ya duniani nzima, hivyo, mkutano huo uliofanyika hapa Beijing ni muhimu sana kwa uchumi wa dunia. Kwenye mkutano huo, mpango wa utekelezaji wa eneo la biashara huria la Asia-Pasifiki umepitishwa, hii inamaanisha kuwa makundi mbalimbali ya uchumi yameanza kupiga hatua ya ufanisi kwa ajili ya kuondoa vizuizi vya biashara kati yao.

    Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng amesema, mpango wa utekelezaji umethibitisha kanuni ya uongozi na hatua za utekelezaji kuhusu kuhimiza ujenzi wa eneo la biashara huria la Asia-Pasifiki, na mpango huo utakuwa waraka wenye mafanikio makubwa katika historia ya APEC.

    Katika kipindi cha mkutano wa APEC, China pia imetangaza kuanzisha mfumo wa njia ya hariri wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 40, ambao utatoa msaada wa kifedha kwa nchi za eneo la uchumi wa njia ya hariri katika ujenzi wa miundo mbinu, uendelezaji wa rasilimali, na ushirikiano wa viwanda. Hatua hiyo pia imepokelewa vizuri na kusifiwa na washirishi wa mkutano huo. Rais Pranab Mukherjee wa Bengal amesema, nchi yake itaunganisha barabara na reli nchini humo na nchi jirani, pia inapanga kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kwenye sehemu ya kati ya nchi hiyo, ili kuifanya Bengal iwe kituo kikuu cha usafiri wa ndege kwenye kanda ya Asia-Pasifiki.

    Katika mkutano wa viongozi wa APEC, rais Xi Jinping wa China alitoa "mpango wa China" kuhusu "ndoto ya Asia-Pasifiki". Amesema, uhusiano wa kiwenzi unamaanisha kuwa, rafiki wanaweza kusaidiana, na kufanya mambo kwa pamoja. APEC inapaswa kutoa mchango katika kuhimiza utandawazi wa uchumi, kuhimiza uzoefu wa mawasiliano, kupinga kujilinda kibiashara, na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia. Wakati huo huo rais Xi Jinping ametangaza kuwa, China itatoa dola za kimarekani milioni 10 katika kuunga mkono ujenzi wa utaratibu na uwezo wa APEC, na ushirikiano wa ufanisi kwenye sekta mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako