Hapa China kuna dada mmoja anaitwa Chen Xiao, yeye huwa anapatikana kwenye internet kwa kuwafanyia watu kazi wanazotaka na anazoweza kufanya. Anatoza karibu dola moja na nusu kwa dakika 8, karibu dola 4 kwa nusu saa na karibu dola 15 kwa saa. Baadhi ya watu wameanza kujiuliza jinsi dada huyu alivyotumia akili na kutumia muda wake kwenye internet kwa faida na sio kupoteza muda.
Pili: Mara nyingi watu wanakuwa wanapoteza muda mwingi kwenye simu na kompyuta wakitembelea tovuti mbalimbali kwa ajili ya kuwasiliana na watu, yaani kuchat, na kasoma habari za burudani na michezo au kununua vitu. Lakini huyu msichana yeye amejitahidi kuitumia internet kwa ajili ya kujiingizia faida. Lakini kuna jambo moja ambalo linashangaza watu, hasa kuhusu jinsi msichana huyo anavyofiriki. Yeye anaona kuwa watu wengi wana maduka ya kuuza vitu, na karibu kila kitu ambacho watu wanataka, tayari kipo madukani, kwa hiyo akafikri itakuwa ni vizuri kama akiuza kitu ambacho wengine bado hawajaanza kuuza, na ambacho kitamsaidia kutumia muda wake vizuri kwenye internet na sio kupoteza bure.
"kwa kuwa siwezi kuongoza maisha yangu vizuri, nikaona ni kwanini nisiwaruhusu wengine waniongoze kila siku? Huko nyuma kila nilipopanga kufanya kitu fulani kwa ajili ya maisha yangu, nilishindwa, ilikuwa inakatisha tamaa sana. Nikafiri kuwa nikiruhusu wengine waniongoze basi huenda nikabahatika kupata kitu kipya na kizuri"
Fadhili: Alichofanya msichana huyu ni kuwa ana duka lake kwenye internet, kama mtu akitaka kumtuma mtu kwenda kununua kitu kama tiketi, au kumwakilisha mahali fulani, au kupeleka kifurushi mahali fulani, basi yeye anaweza kufanya hivyo kwa malipo. Cha muhimu ni kuwa anachoombwa kufanya kinatakiwa kuwa halali na sio uvunaji wa sheria.
Pili: Msichana huyu naweza kusema ni tofauti sana na wasichana wengine wengi wenye umri kama wake, na watu wamekuwa wanajiuliza imekuwaje amefikia hatua ya kufikiri na kutumia muda wake kwenye internet kwa manufaa zaidi kuliko wengine, wakati sasa watu wanalalamika kuwa matumizi ya internet yanawafanya baadhi ya watu wawe wabinafsi na wasishirikiane na wengine. Hili naweza kusema ni tatizo ambalo kwa sasa hata kwenye nchi zetu ambako gharama za internet zimepungua sasa tumeanza kuona watu wakiwa wana chat kwa mwingi, lakini hawafanyi la maana kwenye internet.
Fadhili: kwa sasa hapa China watumiaji wengi wa internet hapa China wanatumia zaidi kwenye simu na sio kwenye computer, hali hii naona imeanza pia kujitokeza kwenye nchi zetu. Lakini kwenye nchi zetu sio wengi waliokuwa na fursa ya kutumia computer wameingia moja kwa moja kwenye internet. Lakini tabia ya kutumia internet kwa njia ya simu inafanana kote, watu wanalalamika kuwa inafanya jamii iwe tofauti na ilivyokuwa zamani. Ule ukaribu wa watu unapotea, siku hizi watu wameanza kuwa na ukaribu zaidi na simu. Hebu tumsikilize Bi Nina kutoka Bujumbura akitueleza jinsi hali ilivyo kwa vijana wa Burundi
Pili: Anachosema Nina sio tu kinawakumba vijana wa Bujumbura, katika miji mingi ya nchi za Afrika hali inakuwa hivi. Kuna baadhi ya watu wanaanza kuwa na wasiwasi kuhusu internet kwenye simu, wengine wanaona simu kuwa ina internet kumewafanya watu wawe na matumizi mabaya, na wengine wanaona ni bora hata iondolewe.
Fadhili: Kuondoa internet kwenye simu labda si jambo la busara. Mfano mmoja mzuri wa manufaa ya internet ni huyo msichana Chen tuliyemtaja. Yeye ametumia vizuri internet kiasi kwamba ameweza kunufaika kibiashara. Kwa hiyo kuondoa internet kwenye simu labda kutapunguza tatizo moja dogo, la muhimu ni kuwepo na namna ya kuwafanya watu waitumie internet kwa manufaa zaidi.
Pili; Hilo naona hata mimi ndio la muhimu, tunatakiwa kuitumia internet kwa manufaa zaidi. Msikilizaji wetu mwingine Bi Adeline wa Katavi Tanzania anapinga wazo la kuzuia internet kwa sababu ya watu wa chache
Pili: Anachosema Bi Adeline ni kweli, tatizo sio simu au internet, tatizo ni tabia ya namna ya kutumia internet. Kwa kiasi fulani inaweza kufanana na msemo wa kuswali "kipya kinyemi". Kutokana na ugeni kwenye kutumia internet watu wanashangaa shangaa tu, wanafanya yale ambayo ni rahisi kwao, lakini ya muhimu ambayo wanatakiwa kusoma kidogo hawaufuati. Hili naweza kusema ni tatizo ambalo labda linaweza kuondoka baada ya muda.
Fadhili: Labda si haki kuwalaumu vijana kwa sasa, maana nakumbuka hata mimi mara ya kwanza kutumia internet nilikuwa mwanafunzi wa sekondari. Kwangu kubwa ilikuwa ni kuangalia habari kuhusu burudani, tena wakati huo tulikuwa tunalipia pesa nyingi sana kwa saa. Kikubwa kwangu ilikuwa ni kuangalia habari za michezo na burudani, wakati mwingine hadi nilikuwa nachelewa kuingia darasani. Lakini hata siku moja nilikuwa siangalii mambo yanayohusiana na masomo . Pamoja na kuwa leo tuko kwenye kipindi hiki tunajarbu kuwalaumu wengine, sijasahau niliyokuwa nafanya nilipokuwa mwanafunzi.
Pili: La muhimu ni kuwa tunatakiwa tufahamu sasa tuna fursa nzuri, na fursa yenyewe tunatakiwa kuitumia vizuri. Internet ni zaidi ya ku-chat, burudani na kuangalia tu picha za nyota. Ina habari za elimu, afya, biashara, utamaduniā¦na kama mtu ukiwa mjanja na kutumia internet vizuri, kama wewe ni mwanafunzi huenda usihitaji kununua kitabu wala kupoteza muda mwili kuandika notes. Masomo kama jiografia, hisabati au biolojia unaweza kusoma mambo mengi kwenye internet. Kama simu yako ikiwa na internet ukiwa mjinga basi utakuwa umejitakia. Na ushauri mzuri tunapewa na msikilizaji wetu Ahmad kutoka Buyenzi Burundi, yeye anaona vijana hata kama wanaitumia kwa mambo ya maana wawe na muda maalum. .
Fadhili: Haya ndio hivyo wengine wanatumia simu wanasahau swala, wengine hata hawaangalii wakiwa njiani karibu wanagongwa, na wengine wakiitwa na wazazi wao hawataki kusikia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |