• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuimarisha mazingira yake ya kibiashara ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi

    (GMT+08:00) 2014-11-20 10:42:06

    Serikali ya Kenya imetangaza kuwa inaendelea na mipango kabambe ya kuboresha mazingira ya kibiashara ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi. Akiongea kwenye ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la kibiashara jijini Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta amesema serikali yake inafanya hivyo kwa kuwa inalenga kuhimiza ongezeko kubwa la uchumi katika miaka michache ijayo.

    Rais Uhuru Kenyatta anasema katika mpango huo wa kuimarisha mazingira ya kibiashara, serikali yake itazingatia miundo mbinu muhimu ya kibiashara na sekta ambazo huchochea kukua kwa biashara. Amesema kwa sasa tayari mipango iko mbioni na inaendelea kutekelezwa, na moja ya mipango hiyo ni kuongeza uzalishaji wa umeme.

    Aidha rais Kenyatta amesema, Kenya imepania kuboresha na kuimarisha kituo chake cha pamoja cha kushughulikia biashara na uwekezaji

    Naye waziri wa utalii, maswala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na biashara nchini Bi. Phyllis Kandie, amesema wawekezaji wanapaswa kuanza kushirikiana na serikali ya kaunti kwa kuwa majimbo hayo kwa sasa ndiyo vitovu vya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako