• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na wajumbe wa mkutano wa mtandao wa Internet duniani

    (GMT+08:00) 2014-11-21 10:20:13

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana mjini Hangzhou alikutana na wajumbe wa China na wa nchi za nje wanaohudhuria mkutano kuhusu mtandao wa Internet duniani.

    Bw. Li Keqiang amesema mtandao wa Internet ni chombo kipya cha kuanzisha biashara na kufanya uvumbuzi, na pia ni jukwaa jipya kwa serikali kutekeleza utawala wake. Amesisitiza kuwa serikali ya China inatilia maanani na kuunga mkono maendeleo ya mtandao wa Internet. Pia amesema China inapenda kushirikiana kwa njia yenye usawa na kunufaishana na nchi mbalimbali duniani katika sekta hiyo kwenye msingi wa kufunguliana mlango na kuheshimiana, ili kutumia kwa pamoja fursa zinazotolewa na maendeleo ya mtandao wa Internet.

    Kwenye mazungumzo hayo, wakurugenzi wa kundi la Thomson Reuters la Uingereza, kampuni ya Qualcomm ya Marekani, shirika la ICANN, kampuni ya Sina ya China, Shirikisho la mtandao wa Internet la China na kundi la Want Want China Times la Taiwan, China walieleza maoni yao kwa niaba ya wajumbe wote zaidi ya 70 wanaohudhuria mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako