• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa ulinzi wa China atoa mapendekezo matatu juu ya usalama wa Asia na Pasifiki

    (GMT+08:00) 2014-11-21 17:40:12

    Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Xiangshang umefanyika Beijing, ukihusisha mawaziri wa ulinzi au maofisa wa kijeshi wa nchi 57 duniani, mashirika manne ya kimataifa pamoja na wataalamu na wasomi jumla ya watu wapatao 330. Waziri wa ulinzi wa China Jenerali Chang Wanquan amehudhuria mkutano huo na kutoa hotuba kuhusu "jeshi la China na usalama wa Asia na Pasifiki".

    Katika hotuba yake, Jenerali Chang Wanquan amesema jeshi la China linapenda kushirikiana na majeshi ya nchi nyingine katika kujenga Asia yenye usalama na pande zote kunufaika na usalama huo na kupata maendeleo kwa pamoja. Jenerali huyo ameeleza sababu ya China kuongeza kasi ya kufanya ulinzi na jeshi uwe wa kisasa, na kusema uwezo wa jeshi la China bado uko nyuma ukilinganishwa na ule wa kiwango cha juu duniani, na maendeleo ya jeshi la China yamekuwa yanadumishwa katika kiwango kinachokubalika. Anasema,

    "hivi sasa, jeshi la China bado lipo katika kipindi ambacho matumizi ya mashine yote bado hayajatimizwa, na hatua za mwanzo za matumizi ya teknolojia ya habari. Bado kuna pengo kubwa kati ya uwezo wa jeshi la China na ule wa kiwango cha juu duniani. Baada ya kuingia katika karne mpya, jeshi la China limeanza kunufaika na ongezeko la nguvu ya taifa, na kuongeza kasi ya kulijenga jeshi kuwa la kisasa, hatua ambayo inalenga zaidi kufanya uwiano kati ya ujenzi wa ulinzi wa taifa na uchumi, na kuhakikisha vizuri maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi na maslahi ya nchi katika nchi za nje. Lakini kinachotakiwa kufahamika ni kuwa China bado haijabadili sera ya kimsingi ya kutoa kipaumbele ujenzi wa uchumi, na maendeleo ya jeshi pia yapo kwenye kiwango kinachokubalika."

    Jenerali Chang Wanquan amesema ushirikiano wa usalama katika Asia na Pasifiki una mustakbali mzuri, lakini njia ya kulinda usalama wa ukanda huo inakabiliwa na changamoto nyingi, kazi ambayo inahitaji juhudi za nchi mbalimbali. Jenerali Chang pia ametoa mapendekezo matatu ya kulinda amani ya kudumu katika Asia na Pasifiki. Anasema,

    "tunapendekeza kuimarisha udhibiti wa migongano, kuongeza uwezo wa kukabiliana na hatari kubwa zinazoweza kutokea; kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika mambo ya ulinzi ili kuongeza hali ya kuaminiana kimkakati na kuimarisha ujenzi wa utaratibu wa usalama wa kikanda na kuhimiza wazo la kuwa jumuiya ya pamoja ya mustakbali.

    Katika mkutano wa wajumbe wote uliofanyika asubuhi ya leo, waziri wa ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Tun Hussein amesema kutafuta ndege iliyopotea ya Shirika la Ndege la Malaysia ni mada isiyoweza kukwepeka, katika kutafuta ndege hiyo, nchi mbalimbali zimnafanya ushirikiano mzuri, jambo ambalo litaweka msingi wa ustawi na utulivu wa kanda ya Asia na Pasifiki. Anasema,

    "nchi tofauti zina teknolojia za aina mbalimbali, kutobadilishana maoni kati ya nchi kutasababisha pengo. Katika kutafuta ndege iliyopotea ya MH370, China na Marekani zimetoa teknolojia na vifaa vyao, na China inatupatia taarifa zilizokusanywa na satilaiti zake, huu ndio ushirikiano. Tunaweza kufanya ushirikiano wa aina hiyo kwa ajili ya maafa,na pia tunaweza kufanya hivyo ili kuchangia ustawi wa kanda yetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako