• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi atoa wito wa kuongeza ushirikiano na New Zealanda kwenye sekta ya kilimo na ufugaji

    (GMT+08:00) 2014-11-21 19:48:23

    Rais Xi Jinping wa China amesema nchi yake na New Zealand zina fursa kubwa ya ushirikiano katika sekta ya kilimo na ufugaji.

    Rais Xi amesema hayo wakati alipotembelea maonyesho ya teknolojia ya kilimo akiwa pamoja na waziri mkuu wa New Zealand, John Key. Amesema kilimo na ufugaji ni sehemu kubwa ya ushirikiano wa pande hizo mbili, na kwamba nchi hizo mbili zina fursa kubwa katika sekta hiyo kutokana na uwezo mkubwa wa kilimo na ufugaji nchini New Zealand, huku China ikiwa ni soko kubwa la bidhaa zinazotokana na sekta hiyo.

    Wakati huohuo, rais Xi Jinping amesema, uhusiano wa China na New Zealand utakuwa na mafanikio zaidi katika siku za baadaye kutokana na juhudi zinazofanywa na watu wa pande hizo mbili.

    Rais Xi amesema, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi miaka 42 iliyopita, China na New Zealand zimeungana na kuendeleza uhusiano wao, ushirikiano wa pande mbili umetoa fursa nyingi za maendeleo ambazo hazijaonekana katika uhusiano kati ya China na nchi nyingine zilizoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako