• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Burkina Faso aliyeondolewa madarakani yuko nchini Morocco kwa muda maalum

    (GMT+08:00) 2014-11-21 19:53:08

    Rais wa Burkina Faso aliyeondolewa madarakani Blaise Compaore amewasili mjini Casablanca, Morocco, ambako atakaa kwa muda maalum.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Morocco imesema, Compaore, akiwa pamoja na watu wengine watano, aliwasili jana usiku nchini humo.

    Taarifa hiyo imesema, Morocco, ikiwa na uhusiano mkubwa wa kihistoria, kibinadamu, na kisiasa na Burkina Faso, imerejea tena uungaji mkono wake kwa mchakato wa mpito unaoendelea nchini humo. Aidha, Morocco inawapongeza watu wa Burkina Faso na jeshi lake kwa moyo wa uzalendo na uwajibikaji walioonyesha katika hatua muhimu ya historia ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako