• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya China yaanza mipango ya kusaidia jamii nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2014-11-21 19:57:50

    Makampuni makubwa ya mawasiliano ya China, ZTE na Huawei yamesaini makubaliano na mashirika ya kiraia ya Kenya yanayolenga kuendeleza elimu ya wasichana, wajasiriamali wanawake, na kupambana na UKIMWI.

    Makubaliano hayo ya kuendeleza maendeleo endelevu yamesainiwa nchini Kenya kwenye hafla iliyohudhuriwa na mke wa rais Margaret Kenyatta.

    Mama Margaret Kenyatta amesema kwa miaka 50 iliopita ushirikiano kati ya China na Kenya umepiga hatua kubwa na manufaa yake yanaonekana katika maisha ya watu kote nchini humo. Naye balozi wa China nchini Kenya Liu Xianfa amesema, China itafadhili miradi ambayo itasaidia kukuza amani na maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako