• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza kasi ya kujenga mtandao wa internet wa broadband

    (GMT+08:00) 2014-11-21 21:06:06

    Naibu waziri wa viwanda na teknolojia ya habari ya China Bw. Shang Bing amesema China itafanya kazi katika maeneo matano ili mtandao wa internet ufanye kazi muhimu zaidi katika kuhimiza ukuaji wa uchumi.

    Bw. Shang ameyasema hayo alipotoa hotuba ya ufungaji wa mkutano wa kwanza kuhusu mtandao wa internet duniani leo mjini Wuzhen mkoani Zhejiang, mashariki mwa China.

    Maeneo hayo ni pamoja na kuongeza ujenzi wa mtandao wa internet wa broadband, kufanya mtandao wa internet utumike katika maeneo mapya yakiwemo viwanda, kilimo, fedha, biashara, elimu, matibabu na huduma za jamii, kufanya uvumbuzi ili kuongeza ushindani wa viwanda vya mtandao wa internet wa China, kuharakisha kukamilisha mfumo wa sheria zinazohusu mtandao wa internet, na kuongeza ushirikiano mpana na nchi mbalimbali kuhusu teknolojia, biashara, vigezo na usimamizi wa mtandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako