• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Obama atangaza mpango wa mageuzi ya uhamiaji

    (GMT+08:00) 2014-11-21 21:06:11

    Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza hatua za kiutendaji kuhusu mpango wa mageuzi ya uhamiaji ambao utawafanya milioni 5 ya wahamiaji haramu nchini humo kuepuka kurudishwa makwao.

    Akilihutubia taifa kupitia televisheni, rais Obama amesema mfumo wa uhamiaji wa Marekani umeharibika na kuna matatizo yasiyotatuliwa kwa muda mrefu, na atatumia madaraka yake kwa mujibu wa sheria ili kuboresha mfumo huo.

    Kwa mujibu wa mpango huo, wahamiaji haramu milioni nne ambao wameishi nchini Marekani kwa miaka isiyopungua mitano wataweza kuepuka kurudishwa nyumbani na wale wasiofanya uhalifu watapata fursa za ajira, na wahamiaji wengine milioni 1 pia hawatarudishwa nyumbani kwa muda.

    Habari zinasema, hivi sasa kuna wahamiaji haramu milioni 11 nchini Marekani, wengi wao wakitokea nchi za Latin Amerika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako