• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatangaza kumalizika kwa maambukizi ya Ebola nchini DRC

    (GMT+08:00) 2014-11-22 20:08:29

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yamemalizika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

    Mwishoni mwa Agosti, DRC ilifahamisha WHO kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo katika wilaya ya Jeera mkoani Equateur. Mlipuko huo uliopelekea watu 66 kuambukizwa ugonjwa huo wakiwemo madaktari 8 hauna uhusiano na maambukizi ya Ebola yaliyotokea Afrika Magharibi. Mlipuko huo ni wa saba kutokea nchini humo tangu virusi ya Ebola vigunduliwa mwaka 1976.

    Wakati huohuo, mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi amesema, vita dhidi ya Ebola vinahitaji pande husika kutekeleza kihalisi ahadi za msaada, na kuanza kufikiria na kuweka mipango ya kuzisaidia nchi zinazoathiriwa na ugonjwa huo kufanya ukarabati wa nchi baada ya maambukizi ya ugonjwa huo kuisha.

    Habari nyingine zinasema, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon amesema, kwa sasa kasi ya maambukizi mapya ya ebola inaonekana kupungua, kama jumuiya ya kimataifa itaendelea kuongeza nguvu ya kukabiliana na Ebola, basi Afrika Magharibi itafanikiwa kudhibiti kabisa maambukizi ya Ebola katikati ya mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako