• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kukuza uhusiano na nchi za visiwa vya Pasifiki

    (GMT+08:00) 2014-11-22 20:19:11

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Fiji leo amefanya mazungumzo na viongozi wa nchi za visiwa vya bahari ya Pasifiki, ambapo ameelezea sera na hatua za China za kukuza uhusiano wa wenzi wa kimkakati na nchi hizo wenye kuheshimiana na kulenga maendeleo ya pamoja.

    Rais Xi Jinping amesema China itatilia maanani zaidi haja ya kuendeleza uhusiano kati yake na nchi za visiwa vya bahari ya Pasifiki na kuongeza uwekezaji kwenye nchi hizo. Ametoa mapendekezo kadhaa ya kuendeleza na kuzidisha uhusiano kati ya China na nchi hizo yakiwemo kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi wa pande zote mbili, kupanua mawasiliano ya utamaduni na kuimarisha uratibu katika jukwaa la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako