• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaidhinisha miradi zaidi ya ujenzi wa reli

    (GMT+08:00) 2014-11-26 18:38:05

    China imeidhinisha miradi ya ujenzi wa njia nne za reli yenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 10 wakati serikali ikijitahidi kuwekeza kwenye miundo mbinu ili kusukuma mbele ukuaji wa uchumi.

    Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China NDRC. Kamati hiyo imefafanua kuwa, njia mpya ya reli itapita kaskazini mashariki mwa mkoa wa Jilin, kusini magharibi mwa Chongqing, mkoa wa Shaanxi na mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani.

    Hii ni mara ya tatu ndani ya mwezi huu kwa China kuidhinisha miradi mipya ya ujenzi wa reli.

    Katika miezi ya hivi karibuni China imeongeza uwekezaji katika miundo mbinu kwa ajili ya kuchochea ongezeko la uchumi wake ambao kasi ya ukuaji wake imepungua kutokana na kudidimia kwa sekta ya uzalishaji na soko la nyumba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako